Skip to main content

UNHCR inasema hatua ya kwanza ya kambi ya wakimbizi wa Ivory Coast imekamilika

UNHCR inasema hatua ya kwanza ya kambi ya wakimbizi wa Ivory Coast imekamilika

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema hatua ya kwanza ya kazi ya ujenzi wa kambi ya wakimbizi wa Ivory Coast mjini Bahn imekamilika.

Hatua hiyo ilikuwa ni kupata eneo, kufanya vipimo na kusafisha eneo la ujenzi lililoko Mashariki mwa Liberia. Kwa mujibu wa UNHCR kambi hiyo itakuwa na makazi 14 yenye uwezo wa kuhifadhi wakimbizi 500 kwa wakati mmoja.

Makambi mengine yatakuwa na vyoo, mabafu, usalama, vutuo vya uandikishaji na ugawaji misaada, jiko, bwalo la chakula, stoo, kituo cha afya, visima vya maji na ofisi kadhaa.