Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanajeshi wa FARDC wakiuka haki za binadamu

Wanajeshi wa FARDC wakiuka haki za binadamu

Ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu imearufu kuwa uchunguzi uliofanywa na mpanho wa Umoja wa Mataifa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO na ule uliofanywa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu katika vijiji vya Kivu ya Kaskazini na Kivu ya Kusini umetoa mwangaza wa ukiukwaji ulikofanywa na wanajeshi wa serikali wa FARDC wakati wa mwaka mpya.

Kwa mujibu wa chunguzi hizo mjini Fizi Kivu Kusini wanawake zaidi ya 30 walibakwa watu wengine kujeruhiwa, huku wengine wakikamatwa na maduka kadhaa kuporwa katikati ya mji huo. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Bwana Colville ameongeza kuwa wanajeshi 14 wamekamatwa kwa kuhusika na uhalifu huo akiwemo Luten Kanal Kibibi Mutware na mameja watatu ambao wote wanashikiliwa katika mahabusu ya jeshi mjini Uvira wakisubiri kesi itakayoanza kusikilizwa hivi karibuni.