Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF, WHO na Bill na Melinda Gates waahidi kutokomeza Polio Angola

UNICEF, WHO na Bill na Melinda Gates waahidi kutokomeza Polio Angola

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, shirika la afya duniani WHO na mfuko Bill na Melinda Gates wamerejea ahadi zao za kuisaidia serikali ya Angola kutokomeza polio nchini humo.

Angola ambayo ilifanikiwa kutokomeza polio kwa miaka mingio imejikuta ikikubwa tena na mlipuko wa ugonjwa huo 2005, na ugonjwa kusambaa katika nchi jirani za Namibia, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Congo Brazzaville kati ya mwaka 2006 hadi 2010.

Ahadi hiyo imetolewa katika siku ya miwsho ya ziara nchini humo ya mkurugenzi mkuu wa UNICEF Athony Lake, Rais wa mpango wa afya wa mfuko wa Belinda na Bill Gates Dr Tachi Yamada na Dr Matshidiso Moeti mkurugenzi msaidi wa Who kanda ya Afrika. George Njogopa na ripoti kamili

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)