Skip to main content

DR Congo, Uganda na MONUSCO kuwasaka waasi wa ADF/NALU

DR Congo, Uganda na MONUSCO kuwasaka waasi wa ADF/NALU

Operesheni ya pamoja ya jeshi la taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uganda na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Congo MONUSCO imeanza mwishoni mwa wiki kuwasaka waasi wa Uganda wa ADF/NALU na makundi mengine ya yenye silaha Mashariki mwa Congo.

Opreresheni hii ni ya awamu ya nne baada ya zile zilizoanza katikati ya mwaka jana katika mistu iliyoko chini yam lima Ruwenzori upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jimbo la Kivu ya Kaskazini. Kama anavyofafanua Meja Celestine Ngeleka afisa wa usimamizi na mawasiliano wa operesheni hiyo kutoka jeshi la serikali ya Congo nia ni kusafisha makundi yote ya waasi Mashariki mwa Congo.

(SAUTI MEJA CELESTINE NGELEKA)