Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP na serikali ya Afghanistan waimarisha msaada wa Chakula

WFP na serikali ya Afghanistan waimarisha msaada wa Chakula

Maafisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Afghanistan na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP wamekutana ili kuweka mkakati wa pamoja wa ugawaji wa chakula cha msaada kinachotolewa na WFP.

Msaada huo unatolewa kwa mamilioni ya Raia wa Afghanistan kwa miaka mitatu ijayo. Mkutano huo ulioandaliwa na makamu wa Rais wa Afghanistan Abdul Karim Khalili una lengo la kuimarisha uratibu wa msaada huo mbaiana ya serikali ya Afghanistan na WFP. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)