Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria lazima ichukue mkondo wake kuhusu Duvalier Haiti:UM

Sheria lazima ichukue mkondo wake kuhusu Duvalier Haiti:UM

Mtaalamu binafsi wa Umoja wa Mataifa Michel Forst leo ameitaka jumuiya ya kimataifa kuruhusu sheria kuchukua mkondo wake nchini Haiti ,akikumbusha kuna kesi ya kusikilizwa dhidi ya mtawala wa zamani wan chi hiyo Jean- Claude Duvalier nchini humo.

Wakati jumuiya ya kimataifa inaunga mkono kurejeshwa kwa utawala wa sheria Haiti, kuunga mkono vita dhidi ya kinga ya makosa ya jinai itakuwa ni ishara nzuri kwa watu wa Haiti na hususani wahanga wa uhalifu huo, amesema mtaalamu huyo aliyeteuliwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuangalia na kutoa taarifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Haiti.

Tanfu mwaka 1986 hadi 2008 hatua za kisheria ziliwasilishwa dhidi ya Jean-Claude Duvalier kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu , utesaji, ubadhilifu wa fedha za umma na vitendo vua uhaini ambavyo vinahalalisha kukamatwa kwake.

Forst ameyasema hayo baada ya kubaini kwamba bwana Duvalier aliachiliwa siku ya Jumanne baada ya kufunguliwa mashitaka ya ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za umma, na kuingilia mfumo wa sheria wan chi hiyo.