Skip to main content

Mkuu wa WHO aelezea mafanikio ya shirika hilo mwaka uliopita

Mkuu wa WHO aelezea mafanikio ya shirika hilo mwaka uliopita

Mkurugenzi wa shirika la afya duniani WHO Dr Margaret Chan amesema kuwa shirika hilo limeshushudia mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za afya ya umma mwaka uliopita.

Akihutubia bodi ya wakurugenzi ya shirika hilo mjini Geneva Dr Chan amerema kuwa chanjo iliyotolewa ya kupambana na ugonjwa wa surua ina uwezo wa kuangamiza ugonjwa huo barani Afrika. Dr Chan pia aligusia masuala ya kupambana na ugonjwa kipindupindu , ukimwi na kifua kikuu lakini akaonya kuwa mashirika mengi yanayohusika na afya ya umma ulimwenguni kwa sasa yanakabiliwa na uhaba wa fedha.