Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WMO yaelezea kwa nini mafuriko Australia,Sri Lanka na Brazil

WMO yaelezea kwa nini mafuriko Australia,Sri Lanka na Brazil

Shirika la kimataifa la hali ya hewa WMO linasema kuwa mafuriko yaliyoshuhudiwa nchini Australia yalisababishwa na adhari za msimu wa La Nina.

WMO hata hivyo inasema kuwa kiwango cha mvua kilichoshuhudiwa hakikutarajiwa mvua ambayo ilisababisha kutokea kwa mafuriko. WMO inasema kuwa bado inaendelea kuchunguza hali za anga nchini Brazil na Sri Lanka kubaini ikiwa mafuriko katika maeneo hayo pia yalisababisha na La Nina. Shirika hilo linasema kuwa msimu wa La Nina unatarajiwa kusababisha kiangazi katika maeneo ya Afrika Mashariki. Omar Baddour ni mtaalamu wa hali ya hewa katika shirika la WMO.

(SAUTI YA OMAR BADDOUR)