Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya milioni moja waathirika na mafuriko Sri Lanka:OCHA

Zaidi ya milioni moja waathirika na mafuriko Sri Lanka:OCHA

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa hadi sasa zaidi ya watu milioni moja wameathirika na mafuriko nchini Sri Lanka.

Pia kumeripotiwa vifo vya watu 27 huku wengine 47 wakijeruhiwa wakati wengine 12 hawajulikani waliko. OCHA inasemakuwa watu 367,000 wako kwenye vituoa 633 katika wilaya 12 wakati wilaya za Batticaloa na Ampara zikiwa na idadi kubwa zaidi ya waathiriwa. Hadi sasa jeshi la Sri Lanka limesafirisha tani 11 za chakula kilichopikwa kwenda kwa maeneo yaliyoathirika.Nalo shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa thuluthi moja ya wale walioathirika na mafuriko hayo ni watoto.