Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EU na shirika la ECHO wasaidia waathiriwa wa mafuri Pakistan

EU na shirika la ECHO wasaidia waathiriwa wa mafuri Pakistan

Idara ya tume ya ulaya inayohusika na kutoa misaada ya kibinadamu ECHO imetoa kima cha euro milioni tano kwa shirikla la kimataifa la uhamiaji IOM zitakazotumiwa kutoa makao ya dharura kwa waathiriwa wa mafuriko ya mwaka uliopita nchini Pakistan.

Mafuriko hayo yaliyotokea wakati wa msimu wa joto mwaka uliopita yalisababisha uaharibifu wa zaidi ya nyumba milioni 1.6. Mashirika ya kutoa misaada yamefanikiwa kutoka makao ya dharura ya mahema kwa watu 783,000 lakini hata hivyo zaidi ya watu maskini nusu milioni hawajapokea msaada huo kama anavyofafanua msemaji wa IOM Jared Bloch

(SAUTI YA JARED BLOCH)

Msaada huo wa ECHO utasaidia karibu familia 15,000 kupata mahema na misaada mingine katika mikoa ya Sindh na Punjap.