UNESCO yafuatilia kazi ya kuhifadhi alipozaliwa Buddha

12 Januari 2011

Mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wenye lengo la kuhifadhi mahala ambapo inasadikika alipozaliwa kiongozi wa imani Buddha huko nchini Nepal umeanza kutekelezwa.

Tayari kundi la wataalamu wa ikolojia limewasili nchini humo kwa ajili ya kufanya ukaguzi utaodumu kwa muda wa miaka mitatu ili kupata uhalisia wa mambo juu ya eneo hilo alilozaliwa Buddha ambalo kwa sasa limechakaa.

Mpango huo wa kufufua eneo hilo linalofahamika kama Lumbini, unaratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO. Kulingana na UNESCO Lumbini ni eneo ambalo linawavutia wahajiri wengi wa madhehebu ya Buddha, na mwaka 1997 UNESCO ililitaja eneo hilo kama eneo muhimu linalotunza urithi wa dunia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud