Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yapongeza utulivu na amani katika kura ya maoni Sudan

UNICEF yapongeza utulivu na amani katika kura ya maoni Sudan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limepongeza hatua ya amani na utulivu iliyojitokeza katika kura ya maoni inayoendelea nchini Sudan.

Shirika hilo limesema linatumai watoto wa Sudan Kusini wataweza kuishi katika mazingira yaliyo huru bila machafuko.

UNICEF imesema inahitaji dola milioni 162.5 kwa shughuli zake za kibinadamu nchini Sudan kwa mwaka huu wa 2011. Merixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MERXIE MERCADO)

Wakati huohuo jumuiya ya kimataifa, muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa wote wamesema mchakato wa kura ya maoni Sudan umeaanza vizuri na wanatumai utamalizika vyema. Kura hiyo itakamilika tarehe 15 Januari na matokeo hayatarajiwi kabla ya Februari. Hata hivyo wote wanaomba matakwa ya watu wa Sudan kuheshimiwa baada ya kura hiyo kukamilika, Tanzania ni moja ya nchi iliyoeleza msimamo wake kuhusu kura hiyo kama anavyofafanua waziri wake wa mambo ya nje Bernad Membe.

(SAUTI YA BERNAD MEMBE)