Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Masuala ya haki muhimu Haiti yanahitaji kutupiwa jicho: UM

Masuala ya haki muhimu Haiti yanahitaji kutupiwa jicho: UM

Katika mkesha wa kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu tetemeko la ardhi lililokatili maisha ya watu zaidi ya 22,000 wakiwemo wafanyakazi 102 wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo ameonyesha mshikamano wake kwa watu wa Haiti na kutoa wito wa juhudi zaidi za kuboresha haki za binadamu kwa watu wa nchi hiyo.

Mkuu huyo amesema anatambua juhudi zilizofanyika na serikali na jumuiya ya kimataifa katika kushughulikia changamoto zinazoikabili nchi hiyo licha ya kupoteza idadi kubwa ya watu. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)