Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 16,000 wasambaratishwa na machafuko ya kikabila Ivory Coast: UNHCR

Watu 16,000 wasambaratishwa na machafuko ya kikabila Ivory Coast: UNHCR

Mapigano ya kikabila yamesambaratisha watu zaidi ya 16,000 Magharibi wa Ivory Coast limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Watu hao wamepata hifadhi katika mji wa Duekoue, Man na Danane. Wakati huohuo idadi ya Waivory Coast wanaoendelea kukimbilia Liberia inaongezeka. Hadi sasa 25,000 wamevuka mpaka na kuingia Liberia. Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR Adrian Edward shirika hilo limeanza kazi ya ujenzi wa kambo mpya ya wakimbizi Mashariki mwa Liberia kwenye mji wa Bahn, kambi ambayo itaweza kuhifadhi wakimbizi 18,000.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

Kwingineko shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeanza kugawa msaada wa chakula kwa wakimbizi wa Ivory Coast walioko Liberia. Na imeandaa chakula cha kuwasaidia watu 200,000 endapo itahitajika.