Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tetemeko la ardhi la Haiti lilitoa changamoto kubwa kwa WFP: Sheeran

Tetemeko la ardhi la Haiti lilitoa changamoto kubwa kwa WFP: Sheeran

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP Josette Sheeran amesema changamoto za baada ya tetemeko kubwa la ardhi nchini Haiti mwaka jana zilitoa mtihani mkubwa kwa shirika hilo.

Amesema ni kutokana na ukubwa wa tetemeko lenyewe, athari zake, na mahitaji ya mamilioni ya watu.

Hata hivyo ameongeza kuwa WFP imeweza kugawa msaada wa chakula kwa watu milioni 4 baada ya tetemeko hilo la Januari 12 mwaka jana na itaendelea kuwsaidia wengine milioni mbili. George Njogopa anaripoti.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)