Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huenda upembe wa Afrika ukawa ngome ya makundi ya kigaidi:Ban

Huenda upembe wa Afrika ukawa ngome ya makundi ya kigaidi:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kutoa msaada wa dharura wa kijeshi na usaidizi mwingine kwa serikali ya mpito ya Somalia ili kuwazuia wapiganaji wa kigeni kulibadili eneo hilo kuwa ngome ya makundi ya kigaidi.

Kupitia kwa ripoti yake kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Ban amesema kuwa suala la usalama bado limebaki kuwa changamoto kubwa kwa serikali ya mpito ya Somalia nchi ambayo imekumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa miaka ishirini. George Njogopa ana taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)