Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban afanya mkutano na waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri

Ban afanya mkutano na waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefanya mkutano na waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri, mkutano unaotajwa kuwa wenye manufaa.

Ban alimpongeza Saad kwa uongozi wake nchini Lebanon hususan wakati wa nyakati ngumu. Wawili hao walijadili masuala kadha yakiwemo ya azimioa 1701 la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na umuhimu wa kuitaka Isreal isitishe mashambulizi yake ya angani. Ban alisisitiza umuhimu wa pande zote mbili kushirikiana ili kuhakikisha kutekelezwa kwa azimio hilo. Kuhusu suala la mahaka maalum Ban alionyesha kuiunga mkono mahakama hiyo na kuongeza kuwa ana matumaini kuwa mahakama hiyo itasaidia kupambana na ukwepaji wa sheria nchini Lebanon. Pia masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na mpango wa amani wa mashariki ya kati na umuhumu wa mpango wa nchi za kiarabu kupata suluhu la mzozo kati ya Israel na nchi za kiarabu.