Skip to main content

Watu zaidi ya 3000 wafariki Dunia kwa Kipindupindu Haiti

Watu zaidi ya 3000 wafariki Dunia kwa Kipindupindu Haiti

Mfumo wa afya nchini Haiti unaosimamiwa na shirika la afya kwa nchi la Amerika PAHO, shirika la afya duniani WHO na wizara ya afya ya Haiti MSPP wameariku kuwa ingawa wana madawa ya kutosha kwa ajili ya kuwatibu waathirika wapya wa kipindupindu siku zijazo lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa.

Mashirika hayo yanasema usambazaji wake katika idara mbalimbali bado ni changamoto, na wakati mwingine hali inazidi kuwa mbaya kutokana na hali ya usalama. Tangu kuzuka kwa ugonjwa huo zaidi ya watu 3000 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 700000 kulazwa hospitali. Sasa serikali inaweka mipango ya kukabili visa vingine 400,000. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)