Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR kuweka kambi maalumu Liberia kwa ajili ya wakimbizi wa Ivory Coast

UNHCR kuweka kambi maalumu Liberia kwa ajili ya wakimbizi wa Ivory Coast

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limesema litaweka kambi maalumu nchini Liberia ili kuwahifadhi wakimbizi zaidi ya 18,000 waliokimbia machafuko nchini Ivory Coast.

Mtaalamu wa mpango wa kambi hiyo ameshawasili Liberia na kazi ya ujenzi wa kambi hiyo mpya utaanza mapema wiki ijayo. Kambi hiyo itajengwa kwenye mji wa mpakani wa Saclepea. Lin Sambini na maelezo kamili.

(SAUTI YA LIN SAMBILI)