WFP inwasaidia watu wanaokimbia machafuko Ivory Coast.
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP inapeleka kwa kutumia ndege msaada wa chakula nchini Liberia ili kuwalisha maelfu ya watu wanaokimbia mgogoro wa kisiasa katika nchi jirani ya Ivory Coast.
Pamoja na chakula kingine WFP inagawa tani tano za biskuti zenye kuongeza nguvu ambazo mara nyingi hutumika wakati wa dharura. Msaada wa kwanza utawsilishwa katika mji wa Saclepea jimbo la Nimba Kaskazini Mashariki mwa Liberia ili kugawanywa kwa wakimbizi. Na shughuli ya ugawaji inafanyika kwa ushirikiano na kamisha mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Jason Nyakundi na ripoti kamili.
(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)