Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame unaendelea kuathiri sehemu kubwa ya Somalia: OCHA

Ukame unaendelea kuathiri sehemu kubwa ya Somalia: OCHA

Msimu wa ukame unaendelea kuathiri sehemu kubwa ya Somalia ikiwemo Somalilanda na Puntland limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA.

Kwa mujibu wa duru za habari ukame huo tayari umesababisha athari kubwa katika maisha ya watu na mifugo hasa kwenye wilaya ya Hobyo mkoa wa Mudug. Hali ya watu pia katika maeneo ya Bay, Bakool na Gedo inazidi kuzorota huku ikitabiriwa kuwa mbaya zaidi endapo msaada wa kibinadamu hautopelekwa.

Watu wameanza kuondoka na kuelekea Moghadishu kuweza kupata chakula na kwenye maeneo ya Juba wafugaji wanakabiliwa na hali ngumu kupata malisho ya mifugo yao. Hali hiyo pia kwa mujibu wa OCHA imesababisha ongezeko kubwa la ombaomba mitaani.