MINUCART yafungasha virago na kuondoka Chad baada ya miaka mitatu

24 Disemba 2010

Ujume au mpango maalumu wa Umoja wa Mataifa Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad MINUCART tarehe 21 wiki hii umefanya hafla maalumu mjini N\'Djamena Chadkukabidhi rasmi jukumu la ulinzi na usalama kwa serikali ya Chad na mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa.

MINUCART kuondoka Chad inafuatia azimio la baraza la usalama namba 1923 la mwezi Mai mwaka huu lililoutaka mpango huo kuondoka ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa Desemba. Tangu mwezi Septemba mwaka huu MINUCART na ofisi ya mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini humo imekuwa ikishirikiana kuhakikisha shughuli ya kukabidhi majukumu inafanyika kwa utulivu na amani.

Lakini nini kilichoisibu MINUCART na hata inaondoka Chad? Na je kuondoka kwao kutaathiri chcochote katika nchi hiyo ambayo ina wimbi kubwa la wakimbizi kutoka Darfur Sudan na pia wakimbizi wake wa ndani. Kujibu haya nazungumza na afisa habari na msemaji wa MINUCART aliyeko Abeche Chad Jumbe Omari Jumbe ambaye kwanza anatoa historia fupi ya MINUCART.

(MAHOJIANO NA JUMBE OMARI JUMBE)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter