Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Ivory Coast atakiwa kutimiza ahadi ya utulivu:UM

Rais wa Ivory Coast atakiwa kutimiza ahadi ya utulivu:UM

Rais mpiganaji wa Ivory Coast ambaye amegoma kuondoka madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi ametakiwa kutimiza ahadi yake na kutoendeleza ghasi.

Laurent Gbagbo anadai ameshinda uchaguzi katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi, lakini jumuiya ya kimataifa ikiongozwa na Umoja wa Mataifa inamuunga mkono mgombea wa upinzani Alassane Ouattara kama mshindi.

Zaidi ya watu 170 wameuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi mwezi Novemba. Mkuu wa masuala ya kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Alain Le Roy anasema,

(SAUTI YA ALAIN LE ROY)

Katika mkesha wa Krismasi ninamtaka asiendeleleze ghasia,kama yeye mwenyewe alivyosema kwenye televisheni siku mbili zilizopita kuwa nataka amani, nawataka wafuasi wangu wote kusitisha ghasia. Hilo lazima lidhihirike na kwa wafuasi wake wote, na lazima liwe bayana.\

Jana Alhamisi baraza kuu la umoja wa Mataifa bila kupingwa limeamua kumtambua balozi aliyeteuliwa na bwana Ouattara kama mwakilishi wa Ivory Coast kwenye Umoja wa Mataifa.