Skip to main content

Baraza la Haki za Binadamu kukutana kujadili hali ya Ivory Coast

Baraza la Haki za Binadamu kukutana kujadili hali ya Ivory Coast

Wakati huohuo baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kesho Alhamisi Desemba 23 itafanya kikao maalumu kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Ivory Coast tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu Novemba 28.

Mkutano huo wa dharura utafanyika kufuatia ombi la serikali ya Nigeria kwa niaba ya kundi la Afrika na Marekani. Wanachama 20 wa baraza la haki za binadamu wameidhinisha kufanyika mkutano huo wakiwemo Ubelgiji, Brazili, Ufaransa, Gabon, Hungary na Japan.

Wengine ni Maldivu, Mexico, Nigeria, Norway, Poland, Jamhuri ya Korea, Marekani, Uingereza na Zambia. Kikao hicho kitatathimini hali halisi na kutoa taarifa maalumu.