Skip to main content

Togo imefuzu kufutiwa madeni ya nje na IMF

Togo imefuzu kufutiwa madeni ya nje na IMF

Taifa la Afrika ya Magharibi la Togo limefuzu msamaha wa madeni wa zaidi ya dola bilioni 1.8 sawa na asilimia 80 ya madeni yake ya nje.

Kihistoria moja ya vikwazo vikubwa vya kuwatoa watu katika ufukara kwenye nchi masikini ni gharama zinazozikabili nchi hizo katika kulipa madeni ya nje. Katika juhudi za kujaribu kuvunja mzunguko usiokwisha wa kulipa riba, katika miaka ya mwisho ya 1990 wawekezaji wa kimataifa walikuja na mpango wa kuzipunguzia madeni makubwa nchi masikini uitwao HIPC.

Mpango huo ni makubaliano baina ya maafisa wa wakopeshaji ulioandaliwa kuzisaidia nchi masikini na zenye mzigo mkubwa wa madeni kuepuka madeni hayo kwa kuwafanya wafuzu kufutiwa, sasa miaka miwili baada ya kuanza mchakato Togo hatimaye imefuzu kufutiwa.