Skip to main content

EU yatoa dola milioni 8 kwa malengo ya milenia Sierra Leone

EU yatoa dola milioni 8 kwa malengo ya milenia Sierra Leone

Kamishna ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya misaada ya kiutu ECHO, imetoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 8.1 kwa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF na serikali ya Sierra Leone kwa ajili ya kufanikisha ufikiaji wa malengo ya maendeleo ya mellenia hasa lengo la upunguzaji vifo vya watoto na uboreshaji sekta ya afya.

Kupitia msaada huo serikali ya Sierra Leone inatazamiwa kuimarisha hatua yake inayozingatia upatikanaji bure wa huduma za afya kwa wote.Jumla ya watoto 60,000 ambao wapo kwenye hali mbaya kiafya watafaidika na mpango huo na pia Wilaya nyingine 12 zinatazamiwa kuunganishwa kwenye mradi huo ambao utafika kwenye maeneo mengine kadhaa.

Mapema mwezi April mwaka jana, Rais Earnest Bai Koroma alizundua mpango wa utoaji huduma bure za afya kwa kinamama wajawazito ikiwa hatua ya kukabiliana na ongezeko la vifo vya kina mama na watoto wadogo.