Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP na IOM kugawa chakula kwa wakimbizi wa ndani Yemen

WFP na IOM kugawa chakula kwa wakimbizi wa ndani Yemen

Mgao wa kwanza wa chakula umewafikia wakimbizi wa ndani katika eneo lililoathiriwa na vita la Al Jawf Kaskazini mwa Yemen.

Mgao huo wa chakula unaotolewa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na shirika la mpango wa chakula duniani WFP,ni wa ngano, sukari, mafuta ya kupigia,mikate na chumvi kama anavyofafanua afisa wa IOM Jemin Pandya.

(SAUTI YA JEMINI PANDYA)

Wakimbizi wa ndani zaidi ya 860 na familia zao kwenye wilaya sita za Kaskazini mwa Yemen ndio waliopata msaada huo.