Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushurikiano utazisaidia nchi kupata samani zake zilizoibwa

Ushurikiano utazisaidia nchi kupata samani zake zilizoibwa

Nchi zinazoendelea zinapoteza kati ya dola bilioni 20 na bilioni 40 kila mwaka kwa sababu ya hogo, ubadhilifu na vitendo vingine vya kifisadi umesema muongozo mpya uliotolewa na Bank ya dunia.

Kwa mujibu wa muongozo huo Asset Recovery Handbook, katika miaka 15 iliyopita ni dola bilioni tano pekee ndizo zilizoweza kupatikana na kurejeshwa katika nchi husika.Sasa muongozo huu mpya unalengo la kusaidia kuziba pengo hilo.

Muongozo huo umetolewa na kitengo cha kurejesha samani zilizoibwa cha Bank ya dunia STRA, katika mradi ulioandaliwa na Bank ya dunia kwa ushirikiano na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC. Na unatoa fursa ya kutambua ni jinsi gani ya kurejesha mali zilizoibwa.

Bank ya dunia inasema kufanikisha hilo lazima kuwe na ushirikiano mkubwa baiana ya wadau, nchi husika, mifumo ya sheria, na mashirika ya umma, na waweze kubalishana taarifa nyeti na washirika wao ili kufuatilia fedha zilizoibwa na kukusanya ushahidi. Pia wawe na uelewa wa sheria zao na nchi wanakokwenda kufuatilia, njia za kuzuia, kupokonya na kurejesha fedha zilizoibwa.