Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usanii unachangia kukua kwa uchumi:UNCTAD

Usanii unachangia kukua kwa uchumi:UNCTAD

Biashara inayohusika na usanii imetajwa kuwa moja ya vitu vinavyochangia kuimarika kwa uchumi.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD.

Ripoti hiyo inasema kuwa mahitaji ya vitu kama filamu , muziki na michezo ya kuigiza ya video vimekuwa na thamani ya juu hata wakati wa hali mbaya ya uchumi.

Imeongeza kuwa iwapo biashara hii itaungwa mkono na serikali basi sekta hii inaweza kutoa mchango mkubwa kwa ukuaji wa uchumi hususan kwenye nchi zinazoendelea. Edna Dos Santos-Duisenberg kutoka UNCTAD anasema kuwa kati ya mwaka 2002 na 2008 mauzo ya bidhaa za usanii yaliendelea kuongezeka na hata baada ya kushuhudiwa kwa hali mbaya ya uchumi mwaka 2008 bishara hiyi ilipanuka kwa asilimia 12.