UM kuchunguza chanzo cha kipindupindu nchini Haiti

UM kuchunguza chanzo cha kipindupindu nchini Haiti

Umoja wa Mataifa unadadisi uwezekano wa kuanzisha jopo la wataalamu wa kimataifa wa sayansi kutanabahi chanzo cha mlipuko wa kipindupindu nchini Haiti.

Kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mipango ya kulinda amani DPKO Alain Le Roy, wamependekeza jopo la kimataifa na wanafanya mazungumzo na shirika la afya duniani WHO.

Amesema lengo ni kupata wataalamu wazuri walio huru ili kuchunguza kwa kina chanzo cha kipindupindu nchini Haiti. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)