Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio la kujitoa muhanga msikitini Iran

Ban alaani shambulio la kujitoa muhanga msikitini Iran

Shambulio la kujitoa muhanga lililokatili maisha ya watu 38 na kujeruhi wengine wengi mjini Chabahar Iran limelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Duru za habari zinasema shambulio hilo limetokea nje ya msikiti wa Imam Hossein Kusini Mashariki mwa Iran.

Katibu Mkuu amesema ameshutushwa na kusikitishwa na kile alichokiita kitendo cha kikatili na cha kigaidi dhidi ya waumini waliokuwa wakisherehekea siku takatibu kwa Washia ya Ashura.