Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waomba hifadhi 27 wafariki dunia kwenye ajali ya boti

Waomba hifadhi 27 wafariki dunia kwenye ajali ya boti

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limeshtushwa na ajali mbaya ya boti iliyotokea kwenye kisiwa cha Chriatmas nchini Australia.

Watu 27 wamekufa na 42 wameokolewa hadi sasa baad ya boti kugonha mwamba na kukatika vipande. Boti hiyo imeelezwa kuwa ilikuwa na waoomba hifadhi takribani 70 raia wa Iran na Iraq, wengi wakiwa wanawake na watoto. Jayson Nyakundi na ripoti kamili.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

Msemaji wa UNHCR Melisa Fleming amesema kuwa hata hivyo ni habari za kutia moyo kuwa hatua za haraka zilipelekea kuokolewa kwa maisha ya zaidi ya abiria 40 lakini hata hivyo wengi zaidi walizama baaada ya mashua hiyo iliyokuwa karibu kutia nanga kupigwa na mawimbi.

Fleming amesema kuwa watu wengi zaidi wanaendelea kupoteza maisha wanapochukua hatua hatari wakikimbia ghasia, dhuluma na umaskini. UNHCR inasema wengi wa wale wanaotumia mashua kuhamia nchi za Asia-Pacific, Mediterranean na Caribbean ni wakimbizi.