Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LRA huenda ikashambulia Dr Congo wakati wa sikukuu:UM

LRA huenda ikashambulia Dr Congo wakati wa sikukuu:UM

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya CONGO MONUSCO leo umetoa tahadhari ya uwezekano wa mashambulizi mapya ya waasi wa LRA wa Uganda dhidi ya raia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati wa kipindi cha sikukuu.

 MONUSCO tayari imeshasambaza wanajeshi wake kama hatua za tahadhari kwenye jimbo la Orientale ambalo siku za nyuma lilishuhudia mashambulio zaidi ya LRA ikiwemo mauaji ya takribani walu 500 siku ya Krismasi mwaka 2008. George Njogopa na taarifa kamili. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Vikosi hivyo kwa hivi sasa vimekuwa vikitoa ulinzi wa ziada kwa mashirika ya utoaji wa misaada ya kiutu,yanayopeleka huduma mbalimbali katika eneo la Kaskazini Mashariki kwa Congo. Hata hivyo MONUSCO inaona kuwa makundi ya kihalifu hasa wapiganaji wa LRA wapo kwenye mkakati wa kufanya mashambulizi kwenye maeneo kadhaa wakati wa sikukuu ya Christmas.

Imeounga mkono pendekezo lilitolewa na Umoja wa Mataifa iliyotaka kuratibiwa kwa mbinu mpya zikazosaidia kuongeza mbinyo kwa makundi hayo na kumaliza hali ya wasiwasi. Tayari kundi hilo la LRA limeripotiwa kufanya mashambulizi kadhaa katika maeneo ya Nambia na Duru.