Hali ya kisiasa Ivory Coast bado ni ya mashaka:Ban

Hali ya kisiasa Ivory Coast bado ni ya mashaka:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anahofia hali ya utata wa kisiasa inayoendelea nchini Ivory Coast ambako matukio kadhaa yanajitokeza yanayoweza kuchochea ghasia.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo Ban amerejea wito wake wa kuzitaka pande husika na wafuasi wao kuwa wastahimilivu na kuepuka vitendo vinavyoweza kuchochea machafuko.

Hali ya sintofahamu imejitokeza baada ya Rais aliyekuwa madarakani Laurent Bagbo kuyakataa matokeo yaliyompa ushindi mpinzani wake Alassane Ouattara baada ya duru ya pili ya kura za Urais Novemba 28.

Maelfu ya raia wameanza kuvuka mpaka na kukimbilia nchi jirani kama Liberia wakihofia usalama wao.