Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya ngojangoja Mwedesha Mashitaka wa ICC awataja vigogo sita waliohusika na machafuko Kenya

Baada ya ngojangoja Mwedesha Mashitaka wa ICC awataja vigogo sita waliohusika na machafuko Kenya

Mwendesha mashitaka mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC Luis Moreno Ocampo, amewataja vigogo sita nchini Kenya ambao wanashutumiwa kwa kuchochea ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu wa Rais mwaka 2007.

Vigogo hao ni pamoja na naibu Waziri Mkuu na Waziri wa fedha wa sasa Uhuru Kenyatta ambaye ametoa kauli hii baada ya kutajwa.

(SAUTI YA UHURU KENYATA)

Wengine ni Waziri wa viwanda Henry Kosgey, Waziri wa zamani wa elimu ya juu William Ruto, Kamishina Mkuu wa zamani wa polisi Hussein Ali, mwandishi wa habari wa radio Joshua Sang na Mkuu wa utumishi wa umma na katibu katika baraza la mawaziri . Francis Muthaura aliyesema.

(SAUTI YA FRANCIS MUTHAURA)

Bwana Ocampo amesema kuna sababu za msingi za kuamini kuwa uhalifu dhidi ya binadamu ulitekelezwa wakati wa machafuko hayo ya Kenya. Ameiomba ICC kutoka kibali cha kuitwa mahakamani watu hao sita ili kukabiliana na mkono wa sheria, na endapo hawatotokea mahakamani basi kibali cha kukamatwa kitatolewa, lakini kwa sasa ni washukiwa hadi watakapopatikana na hatia.

(SAUTI YA MORENO OCAMPO)

Watu zaidi ya 1000 walipoteza maisha katika machafuko hayo, 3500 kujeruhiwa na kuwaacha wengine laki sita wakaachwa bila makazi baada ya siku 30 za machafuko, maelfu walibakwa, na nyumba zaidi ya 100,000 kuharibiwa katika majimbo manane ya nchi hiyo.