Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wakimbizi wa Afghanistan warejea nyumbani: UNHCR

Maelfu ya wakimbizi wa Afghanistan warejea nyumbani: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kazi yake nchini Afghanistan imesaidia kuwarejesha maelfu ya wakimbizi na wakimbizi wa ndani na familia zao katika maisha ya kawaida.

Shirika hilo linasema wiki hii wamepiga hatua kubwa kwa kukamilisha nyumba laki mbili kwa ajili ya wakimbizi wanaorejea nyumbani.

Mpango huo wa makazi nchini Afghanistan ulianza 2002 na umechangia pakubwa kurejea kwa wakimbizi milioni 4.5 katika miaka minane iliyopita. Ingawa umegharibu dola milioni 250, lakini umewafaidi watu milioni 1.4. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)