Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna sababu mpya zinazochangia wimbi la wakimbizi:UNHCR

Kuna sababu mpya zinazochangia wimbi la wakimbizi:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuna ongezeko la wakimbizi kuzikimbia nchi zao kwa sababu tofauti na zile za vita na kukabiliwa na vifo.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya 60 ya shirika hilo hii leo kamishna mkuu wa UNHCR Antonio Guterres ametoa wito wa juhudi za kimataifa kukabiliana na kile alichokiita matatizo ya mapya na yanayoongezeka kwa kasi ya watu kukimbia na kutokuwa na utaifa duniani.

Guterres amesema kuna ongezeko la sababu za kwa nini watu wanaamua kuvuka mpaka na kuingia nchi zingine.

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)

Watu wengi zaidi wanavuka mipaka kwa sababu ya umasikini uliokithiri, kwa sababu ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kwa sababu mahusiano yao na vita. Hivyo kuna wimbi jipya la sababu zinazowalazimisha watu kutawanyika na jumuiya ya kimataifa inahitaji kuweza kukabili changamoto hizo. Nadhani ni muhimu kutambua kwamba hatua za UNHCR zimewapa maisha watu wengi na kuwaokoa na vifo.