Mafanikio makubwa yamepatikana kwenye mkutano uliomalizika Cancun:UM

13 Disemba 2010

Hatua mbalimbali zenye lengo la kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa zimeafikiwa kwenye mkutano wa kimataifa uliomalizika mwishoni mwa wiki mjini Cancun Mexico.

Wadau kwenye mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa wameahidi kuchukua hatua mbalimbali zikiwemo hatua madhubuti kulinda misitu ya dunia na kuanzisha mfuko maalumu wa kufadhimi kwa muda mrefu mikakati ya hali ya hewa ili kuzisaidia nchi zinazoendelea. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Naye katibu mtendaji wa mkataba wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa UNFCCC Christiana Figueres amesema makubaliano hayo yataziweka serikali zote katika uwajibikaji, kwani Cancun imeshatimiza kazi yake.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter