Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana kuleta maoni yao katika Baraza la Usalama.

Vijana kuleta maoni yao katika Baraza la Usalama.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, vijana kutoka mataifa mbalimbali wanatazamia kuzungumza ndani ya chombo hicho kuelezea yale wanayoona ni masuala muhimu yanayozunguka kizazi cha sasa.

Rais wa baraza hilo ambaye pia ni balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice amesema kuwa tukio hilo la aina yake linatazamiwa kufanyika disemba 21 ambapo maoni yatakusanywa kutoka sehemu mbalimbali kabla ya baadaye kuhaririwa na kufikishwa katika chombo hicho.

Kuanzia sasa vijana kutoka kila kona ya dunia wanaanza kutuma ujumbe wao kwa njia ya barua pepe ama mifumo mingine ya mawasiliano, na baadaye ujumbe huo utafanyiwa kazi kabla ya kuchezwa siku hiyo.