Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wahamiaji kuongezeka mara dufu ifikapo 2050:IOM

Idadi ya wahamiaji kuongezeka mara dufu ifikapo 2050:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuwa idadi ya wahamiaji kote dunian inatarajiwa kupanda na kufikia wahamiaji milioni 405 ifikapo mwaka 2050.

Ikitoa ripoti yake wakati wa siku ya kimataifa ya ripoti ya uhamiaji IOM inasema kuwa kuendelea kuongezeka kwa idadi ya wafanyikazi kwenye nchi zinazoendelea na watu wanaoendelea kukimbia athari za mabadiliko ya hewa vitaendelea kuchangia kuongezeka kwa wahamiaji duniani.

Franck Laczko kutoka IOM anasema kuwa nchi zinazoinukia kiuchumi barani Asia , Afrika na Amerika kusini zimekuwa vituo muhimu kwa wahamiaji wanaotafuta ajira.

(SAUTI YA FRANCK LACZKO )

Ripoti hiyo hata hivyo inasema kuwa hata baada ya kuwepo kwa hali mbaya ya uchumi duniani fedha zinazotumwa nyumbani na wahamijia zimeongezeka hadi dola bilioni 316 zilizotumwa kwenye mataifa yanayoendelea mwaka uliopita.