Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kupinga mabomu ya ardhini waanza Geneva

Mkutano kupinga mabomu ya ardhini waanza Geneva

Mkutano wa kimataifa kupinga matumizi ya mabomu ya ardhini yaliyo na athari kubwa umeanza leo mjini Geneva.

Wawakilishi wa nchi wanachama kwenye mkataba unaopiga marufuku matumuzi ya mabomu ya ardhini , mataifa yasiyo wanachama, mashirika ya kimataifa , mashirika ya Umoja wa Mataifa , kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu wanakuta mjini Geneva nchini Uswisi kujadili changamoto zinazokumba kutekelezwa kikamilifu kwa makubaliano hayo.

Mkutano huo wa kumi wa nchi wanachama unaandaliwa mwaka mmoja baada ya nchi wanachama , mashirika ya kimataifa, mashirika ya umma na wengineo kuupitia mkataba huo kwa mara ya pili mjini Cartegana nchini Colombia na kujadili hatua zilizopigwa kutatua suala la matumizi ya mabomu ya ardhini. Jakob Kellenberger ni Rais wa ICRC.

(SAUTI YA JAKOB KELLENBERGER)