Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi imara za amani zatakiwa wakati UM ukiadhimisha siku ya kimataifa ya mshikamano kwa Wapalestina

Juhudi imara za amani zatakiwa wakati UM ukiadhimisha siku ya kimataifa ya mshikamano kwa Wapalestina

Kila mwaka siku ya kimataifa ya mshikamano kwa ajili ya watu wa Palestina inatathimnini hali ya Wapalestina na kufikiria nini kifanyike zaidi kuleta amani ya kudumu.

Akizungumza katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku hii ambayo huwa tarehe 29 November Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuna masuala mawili muhimu yanayofikia wakati nyeti mwaka 2011, kwanza ni Rais wa Palestina Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wameahidi kutafuta na kuafikiana mfumo wa suluhu ya kudumu ifikapo mwezi Septemba na pili uongozi wa Palestina inaelekea kukamilisha ajenda ya kuwa na taifa huru ifikapo mwezi August.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro akiwakilisha ujumbe huo wa Katibu Mkuu amesema Ban amesema anapongeza juhudi zilizofanyika hadi sasa kuimarisha hali ya maisha katika eneo la Palestina, ameutaka uongozi wa Palestina na Israel kutimiza wajibu wao

(SAUTI YA ASHA ROSE MIGIRO)

Siku hii ya mshikamano kwa Wapalestina ilianza kuadhimishwa tangu mwaka 1978, na tarehe 29 Novemba ni muhimu sana kwa Wapalestina kwani mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio tarehe hiyo mwaka 1947 la mamlaka ya Palestina na ya Waisrael na kuwataka majirani hao waishi kwa amani pamoja.