Meya wa Mexico City achaguliwa kuongoza harakati za UM kukabili majanga

Meya wa Mexico City achaguliwa kuongoza harakati za UM kukabili majanga

Bodi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uratibu wa upungazaji wa majanga duniani imetangaza mayor wa Mexico City, Marcelo Ebrard, kuwa mjumbe wake maalumu atayeongoza harakati za kuyaandaa majiji kuwa tayari kwa majanga.

Margareta Wahlström, ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu juu ya masuala ya majanga amemtangaza mayor huyo wakati alipokuwa akihudhuria mkutano wa mamea duniani uliofanyika huko Mexico City na kuongeza kuwa ndiye atayeongoza harakati hizo za kuyafanya majiji kuwa katika hali utayari.

Margareta amesema kuwa Umoja wa Mataifa umeridhishwa na utendaji kazi wa mayor huyo na hivyo hauna shaka ataifanya vyema kazi yake. Wakati wa mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika huko Cancun, Mexico, Bwana Ebrard alifikia maamuzi ya kihistoria pale pale alipoafikiana na mayar wengine kusaini makubaliano ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafu angani.