Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba mpya kupambana na matumizi ya tumbaku waafikiwa

Mkataba mpya kupambana na matumizi ya tumbaku waafikiwa

Nchi ambazo zimeunga mkono mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya upigaji marafuku wa matumizi ya tumbaku zimepitisha mpango mpya wenye lengo kuongeza nguvu ili kukabiliana na matumizi ya tumbaku duniani.

Katika makubaliano hayo mapya nchi hizo zimeridhia mpango ambao utachunguza na kudhibiti marashi yanayonyunyuziwa kwenye tambaku kwa ajili ya kuwavutia zaidi watumiaji.

Wakikutana kwenye mkutano wao wa nne huko Punta Del Este, Uruguay, wajumbe kwenye mkutano huo wameafikiana kuwa, ili kufikia shabaya ya kufanikiwa kupiga marafuku utumiaji wa tumbaku, nchi husika lazima zihakikishe zinaoanisha mipango hiyo ya kimataifa na kuziingiza kwenye mipango ya afya ya kitaifa inayozua matumizi ya tumbaku.

Nchi hizo pia zimeafikiana juu ya ulazima wa kujenga uwezo kwenye maeneo ya utoaji wa elimu, mafunzo na taarifa ili kuongeza uwelewa kwa wananchi kufikia shabaya ya kuzuia matumizi ya tumbaku.