Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nafasi za ajira sekta ya utalii kupanda muongo ujao:ILO

Nafasi za ajira sekta ya utalii kupanda muongo ujao:ILO

Zaidi ya serikali 150, waajiri na waajumbe wa wafanyikazi kutoka zaidi ya nchi 50 wanaokutana kwenye kongamnao la shirika la kazi duniani ILO mjini Geneva wanatarajiwa kujadili maendeleo na changamoto kwenye sekta ya utalii.

Sekta ya utalii ni moja ya sekta kubwa zaiodi zinazotarajiwa kuchangia mapato zaidi na kutoa zaidi ya nafasi milioni 235 za ajira mwaka huu wa 2010 ikiwa ni asilimia nane ya ajira yote duniani. Kulingana na ripoti ya ILO sekta ya utalii iliathirika na hali mbaya ya uchumi iliyoikumba dunia lakini inatarajiwa kuimarika kwa muongo mmoja unaokuja.

Shirika la utalii la Umoja wa Mataifa UNWTO linataraji sekta hiyo kuchangia nafasi za ajira 296 ifikapo mwaka 2019. Mkururegenzi wa shirika la ILO Juan Somavia anasema kuwa sekta ya utalii ina uwezo wa kuwa kiungo muhimu zaidi cha ajira baada ya hali mbaya ya uchumi kuikumba dunia .

Anasema kuwa mchakato kati ya serikali, waaajiri na wafanyikazi utahakikisha kuwa nafasi za kazi zinazopatikana ni za hali ya juu.