Mjumbe wa UM akutana na tume ya uchaguzi Ivory Coast

18 Novemba 2010

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Cost amekutana na maafisa wa ngazi wa juu kwenye tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo kwa ajili ya kujadilia changamoto zilizopo kabla ya duru ya pili ya uchaguzi unaotazamiwa kufanyika mwezi huu.

Mjumbe huyo Y. J. Choi amesema kuwa kwa msingi pande zote kwenye uchaguzi huo zimehaidi kufanya kazi kwa dhati ili kuondoa dosari na kasoro kwa lengo la kufanikisha uchaguzi huo.

Duru hiyo ya pili inatazamia kuwakutanisha Rais Laurent Gbagbo na waziri mkuu wa zamani Alassane Ouattara. Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Novemba 28 kufuatia dura ya kwanza iliyofanyika Octoba 31.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter