Idadi kubwa wajiandikisha kwa kura ya amaoni Sudan:UM
Jopo la Umoja wa Mataifa la kuangalia kura ya maoni ya Sudan Kusini limesema idadi kubwa ya watu wasnapanga foleni kwenye mji wa Wau, makao makuu ya Sudan Kusini kujiandikisha kwa ajili ya kura ya amaoni ya mapema mwakani.
Kura hiyo ya maoani itaamua endapo eneo la Sudan Kusini lijitenge na kuwa taifa huru ama la. Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema jopo hilo linaloongozwa na Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa limezuru mji wa Wau leo Alhamisi.
Amesema wamezuru vituo vitatu vya kuandikisha wapiga kura na kuzungumza na maafisa kwenye vituo hivyo pamoja na watu waliokuwa wamepanga foleni kujiandikisha. Jopo hilo limesema limeshuhudia idadi kubwa ya watu wenye hamasa kwenye vituo hivyo. Wakiwa mjini Wau pia wamekutana na naibu gavana na maafisa wengine wanaosaidia kuendesha kura ya maoni kwenye jimbo hilo.