Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaomba fedha kuwasaidia wahamiaji wa Ethiopia Yemen

IOM yaomba fedha kuwasaidia wahamiaji wa Ethiopia Yemen

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limetoa ombi la msaada wa dola milioni moja ili kusaidia kundi la wahamiaji wa Kiethiopia 1050 walio katika hali mbaya baada ya kukwama Kaskazini mwa Yemen.

Wahamiaji hao ambao ni ehemu ya wahamiaji 2000 wa Kiethiopia walioorodheshwa na kuelekezwa kwa IOM na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, kwenye mji wa mpakani wa Haradh. Wamekwama bila chakula, maji na malazi au njia yoyote ya kuendelea na safari au kurejea nyumbani.

Wahamamiaji hao wanawakilisha tatizo la ongezeko la wahamiaji kwenye mji wa Haradhi walio katika hali mbaya mpakani mwa Yemen na Saudi Arabia. Jayson Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)