Kuvumiliana miongoni mwa jamii ni muhimu sana:Ban
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon leo amesisitiza umuhimu wa kuvumiliana miongoni mwa watu na jamii akisema ni msingi wa amani na utulivu wa kimataifa kwa kuheshimu mila na utamadni.
Amesema ni muhimu lakini zaidi ya yote kuvumiliana ni kitendo cha kuwafikia wengine na kuona tofauti sio vikwazo bali ni karibisho la mazungumzo na kuelewena. Ban ameyasema hayo katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuvumiliana.
Ameongeza kuwa kuvumiliana ni muongozo muhimu katika masuala ya siasa hasa wakati huu ambapo ujinga, kusontana vidole na chuki vinatishia amani na utulivu wa dunia iliyo na jamii tofauti. Amesema leo hii dunia imeletwa pamoja kuliko wakati mwingine wowowte na biashara na tekinolojia lakini cha kwanza ndani ya jamii na mataifa kuna umasikini uliokithiri, ujinga na migogoro.
Na ameongeza kuwa kuvumiliana hakumaanishi kukubali matendo yote na mitazamo , lakini thamani yake ni kutambua na kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa watu wengine.