Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa kulinda jamii wawezekana katika kila nchi:ILO

Mfumo wa kulinda jamii wawezekana katika kila nchi:ILO

Shirika la kazi duniani ILO limesema hakuna sababu kwa nchi yoyote kutokuwa na mfumo muhimu wa kulinda jamii kama mafao ya uzeeni na msaada kwa watoto.

Katika ripoti mpya ILO imesema kwamba mfumo wa kulinda jamii ni nyenzo muhimu kwa jamii ili kupambana na umasikini, kutokuwepo kwa usawa na pia kuwekeza kwa watu mapema na kuwafanya waweze kupata ajira.

ILO imeainisha kwamba wakati hatua za mfumo wa kulinda jamii zimesaidia sana katika kipindi hiki cha msukosuko wa kiuchumi, watu wengi na hasa katika nchi masikini bado hawawezi kupta msaada wa kijamii.

Mkurugenzi wa ILO idara ya msaada kwa jamii Michael Cichon amesema ripoti hiyo baada ya utafiti imebaini kwamba kila nchi inaweza kuwa na mfumo wa msaada wa jamii na kuongeza kwamba hakuna ya sababu yoyote kwa nchi kutiojitahidi kuwa na masuala kama mafao ya uzeeni, msaada kwa watoto wa wasijiweza na masuala mengine ya kuisaidia jamii.